Channel: YahStoneTown
Category: Entertainment
Tags: marcochalimwanafasalamajabirgigy moneymxcartergigi moneysalamanaayyah stonetown yahstonetownjokatekhadijakopadiamondplatnumzfidq
Description: #SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460 ARCTOTIS Imagine siku moja usharekodi video yako kama msanii anaye chipukia alafu unaenda kumuonyesha ‘Boss’ kwa mbwembwe zako zote, pale mezani mwake unamkuta anaangalia video ya msanii mwengine na kuisifia sana, huku akikuambia wewe kwamba ile sasa ndo yenyewe, ndo njia sahihi huku akiwa hata bado hajaiangalia video yako. Utajiskiaje? Utaondoka au utabaki? Utanuna au utaskiliza kwa roho safi na kwenda kuhakikisha unayafanyia kazi yote aloambiwa? Kumbuka pia huyo ambaye umeonyeshwa video yake yeye ana support kibao, support ambayo wewe unaitamani hata robo yake na ki ukweli kwa juhudi zako ukipata basi ilikua kutoboa ni LAZIMA. Hii ni story ya Mauwa Sama ambayo ukimpa sikio au macho na ukamskiliza vizuri basi niamini mimi utakua umefanya jambo la maana sana na nakuahidi utajifunza mengi sana. Mauwa alitokea kupendwa tu na Mwana FA ambaye yeye anamuita ‘God Father’ wake kwa jinsi ambayo alifanya na anaendelea kufanya mengi ambayo yamemueka hapa alipo sana, hapa ambapo mimi na wewe ndo tumepata kumfahamu vizuri na kuwa shabiki yake. Ingawa mimi nakumbuka siku ya kwanza ambayo Mwana FA alinisikilizisha wimbo wa Mauwa ya kwanza ambayo ilibamba huko mkoani Moshi, jinsi Hamis alivyokua anaongea kwa excitement, pale tu niliamini alikua kwenye mikono salama. Baada ya hapo alipovutwa kuja Dar napo pia nlikua na pata kipaumbele cha kuskiliza ngoma zake kabla hazijatoka. Kufanya kazi kwa nguvu, kujitolea, kujitoa na kuchukua risk ni moja ya mashimo ambayo Mauwa aliweza kuyafunika vizuri, humu anatuhadhithia jinsi ambavyo Mama yake alimsaidia kupata ruhusa ya kuja Dar kwa mara ya kwanza kuonana na Mwana FA ambaye alimuambia aje, ila alipofika sio Mwana FA ambaye alimfuata badala yake alikutana na mtu mmoja mrefu mwenye mabega yanayoanzia mlango huu mpaka mlango ule, anasema alishtuka maana hilo halikua tegemeo lake, yeye alijua akifika basi atakutana na Mwana FA na mambo mengine yaendelee kutokea hapo. Purukushani, maneno, scandal, kupanda, kushuka na kupanda tena na tena kwa Mauwa Sama ni khadithi ya kusisimua, na yeye si muongeaji saaana ila kwa kiasi flani tuliweza kupata chochote kitu. Story ya familia yake na masomo ambayo wazazi wake walimkazania ayamalize ndo moja ya silaha zake kubwa kwa sasa, anaamini kwa jinsi ambavyo wazazi walimlazimisha kumaliza masomo hiyo ndo kitu ambacho kinamtofautosha yeye na wasanii wengine kwa umbali mkubwa hasa. Rafiki yangu matumaini uta enjoy na kama ilivyo kawaida yetu pia imani ni kwamba utajifunza kadhaa ambayo yatakusaidia huko mbeleni. Nikutakia Kheri ya Mwaka Mpya, Rafiki. Amani, Salama. Support us through anchor.fm/yahstonetown/support SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs Listen our Podcast on Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack YouTube Link bit.ly/YoutubeSalamaNa Soundtrack Yeah by @MarcoChali youtube.com/watch?v=Cue1HB4fnLQ Follow: Twitter: twitter.com/YahStoneTown Instagram: Instagram.com/YahStoneTown Facebook: facebook.com/YahStoneTown Channel Administered by Slide Digital Instagram: instagram.com/slidedigitaltz